Uwanja wetu Project (UWP) ni mradi mkubwa uliobuniwa na kuanza utekelezaji wake mwaka 2017. Awali ulikuwa mahususi kwa ajili ya kukijengea kiwanja cha mpira wa miguu cha shule kabla ya kubadili wazo na kuamua kukianzisha kiwanja kipya kwa kiwango cha kuta za tofali za saruji kama hatua za awali za kupata kiwanja bora na mazingira rafiki kwa wanamichezo na wanafunzi, lakini pia mazingira rafiki kwa matukio mbali mbali ya ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya na Hata Kitaifa kama vilivyo viwanja vingine vya mijini.
Discover More
BONANZA LA KIPARA PREMIER LEAGUE ni mashindano yaliyoandaliwa na kudhaminiwa na Kituo cha elimu ya watoto cha Sister Jenfrida Academy yaliyoshiriki...
Kuanza kwa Msimu wa kwanza wa mashindano ya UWP SUPER CUP ni ishara ya kuanza kutumika kwa uwanja mpya na wa kisasa kijijini Kipara Mtua ambapo mas...
Historia imeandikwa baada ya ndoto iliyodumu zaidi ya mika sita leo katika Uzinduzi wa uwanja Wetu Project (UWP) Uliofanyika katika kijiji cha Kipa...
Kupata taarifa za mashindano na matukio mbalimbali yanayotarajiwa na yaliyofanyika katika
Uwanja Wetu Project (UWP) na kata ya Kipara Mtua.
1. Kuandaa Mashindano ya Ligi kuu ya UWP itakayo pewa jina maalumu la mashindano hayo.
2. Kuandaa Makongamano na mabonanza ya michezo.
3. Kuanzisha Idara ya kusimamia Michezo ndani ya Kata ya Kipara.
4. Kuandaa kanuni, taratibu na kuingia mikataba mbali mbali ya Kimaslahi.
5. Kutoa gawio la faida kwa jamii.