UWANJA WETU PROJECT

  • 2023-11-04
thumb

Historia imeandikwa baada ya ndoto iliyodumu zaidi ya mika sita leo katika Uzinduzi wa uwanja Wetu Project (UWP) Uliofanyika katika kijiji cha Kipara Mtua, Nachingwea baada ya kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa wilaya ya Nachingwea kushuhudia kile kilichokua kinaaminika hakiwezekani na kimewezekana. Sherehe hizi za uzinduzi zimehudhuriwa na wageni mbali mbali wa wilaya ikiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mh. Mohammed Moyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Ndugu Adinani Mpyagila, Maafisa utamaduni wilaya, Viongozi wa Chama cha Mpira wilaya (NAFA), Afisa Tarafa Naipanga, waheshimiwa Madiwani toka kata mbali mbali, watendaji kata, watendaji wa vijiji na vitongoji huku uzinduzi ukipambwa na Burudani kutoka vikundi mbali mbali ndani na nje ya wilaya. Tukio limevuta hisia za watu wengi hasa wapenda michezo na kuona ni dhahiri shahiri kwamba Kipara inakwenda kuwa kitovu cha burudani za soka ndani ya wilaya. Tukio la uzinduzi wa uwanja katika Hatua ya Kwanza ya utekelezaji mradi ilianza kwa Mkuu wa wilaya kupanda mti wa ukumbusho alama itakayosimama daima kwenye historia ya Uwanja. Ni juhudi za vijana walioamua kujiunganisha na kutengeneza kikundi chenye lengo la kujenga kiwanja cha michezo kwa burudani.