Kuanza kwa Msimu wa kwanza wa mashindano ya UWP SUPER CUP ni ishara ya kuanza kutumika kwa uwanja mpya na wa kisasa kijijini Kipara Mtua ambapo mashindano haya yatakuwa yakifanyika kila mwaka muda na wakati huu wa majira ya baridi hasa hasa mara baada ya mavuno jamii itakua ikipata nafasi ya kufurahia burudani za soka. Ufunguzi wa mashindano haya yalitanguliwa na mechi za ngao ya hisani ambapo fainali yake ilifanyika tarehe 12/05/2024 yakifunguliwa na Mheshimiwa Diwani kata ya Kipara mtua Ndugu. Peter Mbonde. Michezo ni nguzo imara katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza na ni nguzo bora kwa uchumi endelevu ni safari ya kukifanya kijiji cha kipara Mjini kuwa Kisiwa cha Burudani. Tukio la uzinduzi wa ligi hii kubwa ya ukanda huu iliambatana na burudani za wasanii mbali mbali ya bongo fleva na Singeli michano waliyoipamba na kuinakshisha siku hii. Mashindano ya UWP SUPER CUP imepata bahati ya kushiri Timu 13 kutoka maeneo mbali mbali ndani na nje ya kata ya kipara Mjini ambazo ni Super Eagle FC, Stand FC, Totenham Spurs, New Castle, Mtua FC, Manowari FC, Mamelodi FC, Moto wa Gesi FC, Sentry FC, Ntila Star, Nalengwe City, Ilala boys FC na Farm 8 FC. Ligi ilimazika kwa mchezo wa fainali kati ya Super Eagle FC na Mtua Star kutoka kijiji cha Mtua. Zawadi mbali mbali zilitolewa kwa washindi kama vile Ng'ombe, mbuzi, Medali za dhahabu, Fedha na shaba, pesa taslimu, Kiatu cha Dhahabu, mkono wa dhahabu, na zawadi ya Kombe la Dhahabu. Kumalizika kwa mashindano haya ni mwanzo nzuri kwa maandalizi ya msimu wa pili wa 2025.