MALENGO YETU

MALENGO YETU

MALENGO MENGINEYO YA UWP

Licha ya kuwako na lengo hilo kuu lakini bado yalikuwako malengo mengine madogo madogo ya mradi huu wa UWP, malengo hayo ni:

1.  Kuwajengea mazingira salama na rafiki wanafunzi.

Kabla ya wazo hili kubadilika na kuamua kuanzisha uwanja mpya kabisa, moja ya lengo lilikuwa ni kuwasaidia wanafunzi kupata eneo lenye wigo ili kukinga dhidi ya ajali za barabarani wakati wakishiriki michezo jioni au asubuhi ukizingatia uwanja huu upo karibu sana na baba bara kuu.

2.  Kuwa sehemu ya chanzo cha mapato

Lengo la pili la mradi huu wa UWP ni kuwezesha na kuwa sehemu ya chanzo kikuu cha mapato kwa shule, serikali, vilabu na wawekezaji kupitia viingilio vya matamasha na michezo mbali mbali kisha kuwa lango kuu la kiuchumi kwa wote.

3.  Kuwa fahari kwa kanda ya Magharibi mwa Nachingwea

Kupitia mradi huu lengo la tatu ni kuwa wa mfano bora kwa kanda yetu ya kilimarondo lakini pia kuwa walimu kwa wengine kuwadhihirishia ni namna gani tukiamua kama jamii tunaweza. Pia itasaidia kukitangaza kijiji na kata ya Kipara kwa wengine hasa uwanja huu utakapoteuliwa kama kituo rasmi kwa mashindano ya kiwilaya, Mkoa, na hata Matukio ya kitaifa.

4.  Kuondoa tatizo la dhana ya utegemezi katika kufikiri na kusubiri kila jambo litoke kwa serikali na kufanywa na serikali.

Mradi huu utakapokamilika utatoa majibu sahihi ya usemi wa kwamba “Tukiamua tunaweza” pia itatoa mwanga kwa ushawishi wa miradi mingine kuibuliwa na kuendeshwa hadi mafanikio ya tamati kupitia uibuliwaji na usimamizi wa wazawa wenyewe.

Ili kuweza kuufanikisha mradi huu, njia mbali mbali zilipendekezwa za kuzitumia na kuyafikia malengo haya, miongoni mwa mapendekezo hayo ni haya hapa:-

i)  Serikali ya Kijiji au Kata kwa kushirikiana na kamati ya shule wakae na kukubaliana namna nzuri ya kutoa zabuni kwa watu binafsi wanaopenda kuwekeza na kuujengea uwanja.

ii) Uwanja kuugawa katika vipande sawa kadiri ya idadi ya timu zilizopo katani ili kila timu ihusike kuujengea kwa mgawanyo wa faida.

iii) Nguvu ya serikali katika kuwashauri wananchi wake kuchangia jambo la kimaendeleo na kuufanya kama mradi wa kijiji/kata.

Hizi ndizo zilikuwa njia kuu tatu ambazo zilipendekezwa kupitia waraka huo. Baada ya kuuwasilisha waraka huo kwenye kikao cha wajumbe wa halmashauri ya kijiji njia namba (i) ilipata kura nyingi na kuungwa mkono na wajumbe walio wengi kwa kura za ndio kama njia bora na rahisi itakayo harakisha ujenzi wa uwanja endapo wadau watapatikana.

Wafadhili na Washirika
thumb
thumb
thumb
thumb
thumb
thumb
thumb
thumb