UWANJA WETU PROJECT

  • 2024-11-09
thumb

BONANZA LA KIPARA PREMIER LEAGUE ni mashindano yaliyoandaliwa na kudhaminiwa na Kituo cha elimu ya watoto cha Sister Jenfrida Academy yaliyoshirikisha timu chache kutoka ndani ya kata ya Kipara Mtua lengo likiwa ni kuendeleza vipaji vya wanamichezo ili kukuza maarifa. mashindano haya yalihusisha utoaji wa zawadi za Fedha na Kombe Trophy lakini yanatoa ofa kwa Timu iliyoshinda kusafiri na kwenda kushuhudia mechi moja ya Namungo FC ya ligi kuu Bara NBC premier mjini Ruangwa katika uwanja wa majaliwa Stadium ili kujifunza namna timu zilizofanikiwa wachezaji wao wanavyocheza.