Uwanja wetu Project (UWP) ni mradi mkubwa uliobuniwa na kuanza utekelezaji wake mwaka 2017. Awali ulikuwa mahususi kwa ajili ya kukijengea kiwanja cha mpira wa miguu cha shule kabla ya kubadili wazo na kuamua kukianzisha kiwanja kipya kwa kiwango cha kuta za tofali za saruji kama hatua za awali za kupata kiwanja bora na mazingira rafiki kwa wanamichezo na wanafunzi, lakini pia mazingira rafiki kwa matukio mbali mbali ya ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya na Hata Kitaifa kama vilivyo viwanja vingine vya mijini.
Wazo hili la ujenzi wa uwanja ni matokeo ya shauku ya muda mrefu ya kutaka ndani ya kijiji cha Kipara kuwa na Uwanja mkubwa uliojengewa kama ilivyo kwa viwanja vingine vya serikali, taasisi na vyama.
Uwanja Wetu Project utahusisha wadau binafsi, taasisi binafsi au serikali na mashirika yake ambao watakua na moyo wa kujitoa na kudhamini. Utekelezaji na ukamilishwaji wa mradi huu mpaka kufikia tamati kwa hatua ya kwanza unatarajia kutumia muda sio chini ya miezi kumi na nane kuanzia mwezi Disemba 2017 hadi Aprili 2020.
Mfumo mkuu utakaotumika ni njia ya kuwekeza kwa Hisa, ambapo mchangiaji hatakuwa na kikomo kadiri ya pato lake.
Karibu UWP weka akiba kwa maisha ya sasa na ya baadae.